Thursday, November 5, 2009
WIZI MTUPU! FIRE EXTINGUISHER MOJA KUKAGULIWA TSHS 5000!
Bongo sasa inabidi watu tusimame tupiganie haki zetu... Yaani kukaguliwa Fire extinguisher moja ya gari aina yoyote Idara ya Zimamoto hapo Fire ni Tshs 5,000/= ? Hivi dar kuna magari mangapi, piga hesabu ya magari yote hayo mara 5000.
Hilo pato linalopatikana hapo linaenda wapi? Litatutengenezea barabara zetu au ndio tena kwenda ktk mifuko ya watu?
Hivi hizi bei zinapangwa na nani?
Kwa mawazo yangu binafsi Tshs 2000/= ingetosha kwa huo ukaguzi tena hata ikiwezekana tutozwe buku tu (1000/=).
Najua kuna wadau wanawaza dah... Angel anamind buku tano! Ndio bwana, haki bin haki kwa mwenye nacho na asiye nacho!
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
No comments:
Post a Comment