Pages

Tuesday, December 8, 2009

My Message to the streets :-)



Happy Independence Day 9th December, 2009.

Uonevu, Unyang'anyi, Umwinyi... yale yote yaliyopingwa ndio yamejaa katika jamii ya watanzania ya leo, mwenye nacho ni Mungu wa asiyenacho, Usawa imekuwa ndoto, tajiri anayefuata uzazi wa mpango mke mmoja, watoto wawili, nyumba kumi, magari sita na mabilioni kujilimbikizia ya kodi zetu wanyonge!

Masikini milo miwili kwa siku imekuwa ndoto, chai asubuhi kitendawili inabidi chai inywewe mida ya saa nne asubuhi kukata makali ya mlo wa pili wa saa kumi na moja jioni na ndio lala salama... kama kuna watoto basi ndio uji wa mchana tena sembe halina blue band wala maziwa.

Je Tutafika?